April 30, 2025 04:56:04 AM Menu



 KIUNGO wa Klabu ya Rangers ya Scotland, Joey Barton anakabiliwa na adhabu kwa kucheza kamari kinyume na sheria za soka nchini humo.
Barton anatuhumiwa na chama cha soka nchini Scotland (SFA) kwa kuweka dau mara 44 kati ya Julai 1 na Septemba 15, mwaka huu.
Barton atarejea katika klabu hiyo baada ya kufungiwa kwa wiki tatu kutokana na utovu wa nidhamu.
Chama cha soka nchini humo, kupitia sheria yake kifungu cha 33 inakataza wachezaji, makocha, maofisa wa klabu na waaamuzi nchini humo kuweka dau kuhusu matokeo ya michezo popote pale duniani.
 Mei mwaka huu kiungo wa Partick Thistle, Steven Lawless alifungiwa michezo sita baada ya kuthibitika kuwa alicheza kamari ya michezo 513.

06 Oct 2016

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top