AZAM ikiwa
mwenyeji kwenye Uwanja wa Uhuru mbele ya Yanga imeshindwa kubakiza alama tatu
baada ya mchezo wao kumalizika kwa sare ya bila kufungana.
Mchezo huo
ambao ulijaa ubabe mwingi, ulishuhudia mwamuzi Israel Nkongo akitoa kadi za
njano tano huku nne zikienda kwa Azam na moja kwa Yanga.
Katika
mchezo huo washambuliaji wa Yanga wakiongozwa na Donald Ngoma wa Yanga na wale
wa Azam waliokuwa chini ya nahodha John Bocco walikosa nafasi nyingi za kufunga
mabao lakini uwezo wa makipa wa timu zote uliwafanya washindwe kutikisa nyavu
zao.
Takwimu
zinaonyesha Azam walicheza faulo 17 na Yanga 10, mashuti yaliyopigwa na Azam na
kulenga lango yalikuwa matano kwa Azam na Yanga sita.
Post a Comment