SERIKALI ya
Tanzania imezuia Klabu za Simba na Yanga kuzitumia Uwanja wa Taifa kutokana na
uharibifu uliofanyika jana katika mchezo wa ligi kuu uliozipambanisha timu hizo
ambazo zilitoka sare ya bao 1-1.
Waziri
mwenye dhamana ya michezo nchini, Nape Nnauye ametangaza kuufungia uwanja huo
leo kwa timu za Simba na Yanga mpaka pale watakapofanya maamuzi mengine hapo baadaye.
Aidha
alisema Simba itatakiwa kulipia hasara iliyotokana na uharibufu huo ambapo viti
zinakadiriwa kuywa 1781 vilivunjwa huku akiongeza kuwa watafunga kamera za CCTV
uwanja nzima ili kufuatilia mienendo ya mashabiki wanapokuwa uwanjani.
“Uwanja huu
hautatumika kwa Yanga na Simba mpaka tutakapoamua hapo baadaye, watafute
viwanja vingine, hapa kuna pesa za walipa kodi, pesa za Watanzania na
wanaotakiwa kuutumia uwanja huu ukiwa mzuri kama ulivyo ni wengi kuliko Yanga
na Simba wako wengine ambao ni wastaarabu wanaweza kuutumia uwanja huu,” alisema
Nape.
Post a Comment