MWENYEKITI
wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji ametangaza kuahirishwa kwa mkutano wake na
wanachama wa klabu hiyo uliotarajiwa kufanyika kesho Jumapili kufuatia kupokea
barua ya zuio la mkutano huo kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Wanachama
wawili wa klabu hiyo Juma Magoma na aliyewahi kuwa mwansheria wa klabu hiyo,
Frank Chacha ndiyo walioiomba mahakama hiyo izuie mkutano huo uliopangwa
kufanyika kwenye Makao Makuu ya klabu hiyo yaliyopo Jangwani jijini Dar.
Manji
ametoa tamko hilo la kuahirisha kwa mkutano huo limetolewa leo kwenye makao
makuu ya klabu hiyo na kudai kuwa hawezi kuingilia uhuru wa mahakama kwani
anaamini suala hilo litaisha na atatangaza tarehe nyingine ya kufanyika kwa kwa
mkutano huo mara baada ya taratibu zote za kimahakama kukamilika.
Aidha
Manji amewataka wanachama wa klabu hiyo kuwa wavumilivu huku akiwaomba
wanachama waliokuwa watokee mikoani kuacha kuja jijini Dar es Salaam hadi hapo
atakapotangaza upya.
Post a Comment