YANGA leo imeendelea kuisogelea Simba baada ya leo kupata ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Toto African katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Ikicheza soka la kuonana Yanga yenye alama 18 huku Simba wakiwa kileleni na pointi zao 23, iliandika bao la kwanza kunako dakika ya 28 kupitia kwa Mzambia, Obrey Chirwa akiunganisha vyema pasi ya kiungo mshambuliaji Simon Msuva ambapo alifunga bao kwa kichwa cha ‘kuchumpa’.
Baada ya bao hilo kuingia, Toto walikuja juu na kuliandama lango la Yanga lakini uimara wa mabeki wa kati Kelvin Yondani na Dante pamoja na wale wa pembeni, Oscar Joshua na Hassan Kessy uliwazima washambuliaji wa Toto waliokuwa wakihaha kusawazisha.
wachezaji Yanga wakishangilia kwenye moja ya mechi zao

Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, Yanga ilitoka kifua mbele na bao hilo moja. Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo dakika ya 54 Jamal Soud alimfanyia madhambi kiungo mshambuliaji wa Yanga, Deus Kaseke aliyekuwa akienda kuonana na Deogratius Munish na mwamuzi kuamuru penalti.
Penalti hiyo ilipigwa kiufundi na Msuva na kujaa wavuni hivyo Yanga kuandika bao la pili. Baada ya hapo timu zote zilifanya mabadiliko kadhaa ambayo yalionekana kuamsha upya mchezo huo lakini hadi mwisho Yanga 2-0 Toto.
Takwimu zinaonyesha Toto walipata kadi za njano mbili na Yanga hawakupata, kwa upande wa mashuti yaliyolenga lango Toto walipiga matatu kama ilivyo kwa Yanga. Aidha wenyeji waliotea mara tatu na Yanga mara mbili. 

Post a Comment

 
Top