MIAMBA ya soka kutoka Italia, AC Milan
imepanga kuimarisha kikosi chake msimu huu katika usajili wa dirisha dogo kwa
kumsajili winga wa Man United, Memphis Depay, 22.
AC Milan ambayo kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya
Italia ‘Serie A’ ipo nafasi ya sita ikiwa na alama 10 baada ya kushuka uwanjani
mara sita, inahaha kuhakikisha inaboresha kikosi chake hususan kwenye safu ya
ushambuliaji kwenye majira ya baridi yaani Januari mwakani.
Mtandao wa Tuttomercato umeripoti kuwa chaguo
la kwanza katika maboresho hayo wameonekana kumgeukia Depay ambaye amekuwa
hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara tangu atue Man U msimu uliopita
akisajiliwa na Louis van Gaal na hadi sasa akiwa chini ya Kocha Jose Mourinho.
AC Milan pia inaonekana kuvutiwa kumsaini
kiungo wa Chelsea, Oscar, 25.
Post a Comment