BAO la kusawazisha la dakika 87
lililofungwa na Shiza Kichuya dhidi ya Yanga wikiendi iliyopita, wachezaji na
mashabiki wa Simba walilifurahia, lakini kwa upande wa wapinzani wao lilivuruga
mipango ya timu hiyo ya kulitetea taji lao la Ligi Kuu Bara.
Kichuya, alifunga bao wakati timu yake
ipo nyuma kwa bao 1-0 hadi dakika hiyo baada ya kupiga kona iliyozama moja kwa
moja wavuni baada ya kumshinda kipa Ali Mustapha 'Barthez’ na kufanya mechi
hiyo kuisha kwa sare ya bao 1-1.
Sare hiyo iliiwezesha Simba kuendelea
kukaa kileleni kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 17 huku Yanga wakiwa na
11 katika nafasi ya tano.
Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm,
alisema matokeo hayo ya sare na Simba yameshusha moraliya wachezaji wake ambayo
awali ilikuwa juu.
Pluijm alisema, katika mechi hiyo
benchi la ufundi na wachezaji wa timu hiyo, walikuwa wakihitaji pointi tatu ili
kuipunguza kasi Simba ambayo haijapoteza hata mechi moja katika mechi saba
ilizocheza.
"Nikiri kabisa kuwa, matokeo ya
sare ya bao 1-1 tuliyoipata kwenye mechi iliyopita na Simba, yameshusha morali
yote ya wachezaji wangu.
"Kwani kwenye mechi hiyo,
tulihitaji ushindi ili tupunguze kasi ya Simba ya kupata matokeo mazuri na hilo
ndilo lilikuwa lengo letu ambalo lilishindikana baada ya kusawazisha bao dakika
za majeruhi.
Post a Comment