KASI
kubwa ya kuzifumania nyavu ambayo mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga raia wa
Zambia, Obrey Chirwa ameanza kuionyesha hivi karibuni katika michuano ya Ligi
Kuu Bara imewafanya wale waliokuwa wakimpuuza awali kuwa hana lolote kufuta
kauli zao na kuanza kumuombea mema kwa Mungu.
Mmoja
kati ya watu hao ni Mzee Ibrahim Akilimali ambaye siku chache baada ya Chirwa
kutua nchini alianza kumponda kuwa hana lolote na kiwango chake siyo cha
kuitumikia timu hiyo, hivyo Yanga imepoteza fedha zake kwa kumsajili.
Hata
hivyo, juzi Jumatano wakati Akilimali akizungumza na Championi Ijumaa alifuta
kauli zake hizo alizokuwa akizitoa kwa Chirwa baada ya kusema kuwa alikuwa
akifanya hivyo kwa lengo ya kumjenga ili aongeze bidii uwanjani.
Alisema
kwa sasa anafurahishwa na kiwango cha mshambuliaji huyo, kwani hivyo ndivyo
alivyokuwa akitaka afanye kwa faida ya timu ambayo ilimsajili kwa mamilioni ya
fedha kuliko mchezaji mwingine yeyote klabuni hapo.
“Ujue
watu walikuwa wananielewa vibaya lakini lengo langu lilikuwa ni kumfanya
aongeze bidii na sikuwa na nia nyingine dhidi yake.
“Lakini
kwa sababu ameanza kufanya kazi tuliyokuwa tukiikusudia kutoka kwake, sina tena
tatizo naye na sasa namuombea kwa Mungu aendelee kufanya vizuri, kama kulikuwa
na watu wamemfunga miguu basi washindwe,” alisema Akilimali.
Mpaka
sasa, Chirwa amefunga mabao matano kwenye mechi nne alizoanza katika kikosi cha
kwanza cha timu hiyo.
Post a Comment