KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva,
amesema anampa asilimia kubwa straika wa timu hiyo, Mrundi, Amissi Tambwe
kuibuka mfungaji bora mwishoni mwa msimu kutokana na kasi anayoionyesha katika
kuzifumania nyavu.
Tambwe jana aliufunga bao moja na hivyo kufikisha
mabao saba moja pungufu dhidi ya kinara Shiza Kichuya mwenye nane.
Msuva amesema, kwa hali jinsi ilivyo hivi sasa
ndani ya kikosi chao, kila mshambuliaji ana uchu ya kufumania nyavu ili mwisho
wautwae ubingwa lakini kuhusu ufungaji bora amempa nafasi kubwa zaidi Tambwe.
Hadi kabla ya mchezo wa jana, Yanga ilikuwa na
wafungaji wanne ambao wapo katika nafasi nzuri ya kuwania ufungaji bora akiwemo
Msuva 5, Obrey Chirwa 5 na Donald Ngoma 4.
“Kila mmoja ndani ya kikosi cha Yanga anafunga
kwa kuwa kila mtu anahitaji kuisaidia timu yake, katika suala zima la kuibuka
na kiatu cha dhahabu nampa nafasi hiyo Tambwe kutokana na ujuzi wake katika
kufumania nyavu.
“Mfano mzuri unaonekana ndani ya kikosi chetu
kuna mwenye mabao sita, matano na manne, hii inaonyesha ni jinsi gani
tunahitaji kutwaa ubingwa na ni matumaini yangu tutafanya vizuri lakini Tambwe
ana nafasi nzuri zaidi kutokana na kasi yake,” alisema Msuva.
Post a Comment