April 11, 2025 06:01:47 PM Menu




HOFU? Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm ameibuka na kusema mchezo wao ujao dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa Jumamosi ya wiki hii hautakuwa rahisi kwani wapinzani wao siyo watu wa mchezo-mchezo.
Pluim ambaye amekiongoza kikosi hicho jana kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Toto ameonekana kuingiwa na hofu juu ya mchezo huo lakini amesema watapambana ili kuondoka na ushindi.
“Naifahamu Kagera siyo timu ya mchezo kwani iko imara na sisi tutacheza nao huku tukitambua wazi kuwa wako vizuri lakini tutahakikisha kuwa tunashinda mchezo huo,” alisema Pluijm.
Yanga na Kagera watacheza kwenye Uwanja wa Katiaba ambao umeboreshwa.



20 Oct 2016

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top