SIMON
Msuva juzi Jumamosi alifunga bao lake la 52 katika kikosi cha Yanga na baada ya
mchezo akasema bao lake hilo amempa mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji
kutokana na uongozi wake uliotukuka.
Msuva
alikuwa kwenye ubora wa juu wakati Yanga ikiichapa Kagera mabao 6-2 katika
Uwanja wa Kaitaba na licha ya kufunga bao hilo, alitoa pasi za mabao (asisti)
mengine manne.
Msuva
alisema kutokana na mwenyekiti wao Manji kuiongoza timu hiyo kwa mafanikio
makubwa, basi anamzawadia bao lake hilo la 52.
“Naushukuru uongozi wa timu yangu ya Yanga kwa
kutuwezesha na kutusapoti lakini niseme kuwa bao langu la leo (juzi), nampa
mwenyekiti wetu Manji iwe kama zawadi ya uongozi wake kwetu,” alisema.
Msuva
amesema bado ana ndoto za kufunga mabao mengi kwa faida ya timu.
“Bado ninahitaji kuvunja rekodi nyingi zaidi
katika timu yangu, hivyo nitaendelea kujituma ili niweze kufanikiwa zaidi
kupitia soka,” aliongeza.
Hadi
sasa Msuva ana mabao manne msimu huu. Itakumbukwa kwamba aliwahi kuibuka
mfungaji bora Bongo msimu wa 2014/15 baada ya kufunga mabao 17. Kwenye Kombe la
Mapinduzi 2015 visiwani Zanzibar pia aliibuka mfungaji bora akifunga mabao
manne.
Post a Comment