SKENDO ya
madawa ya kulevya imekuwa ikimtesa kwa muda mrefu beki wa kushoto wa Yanga,
Haji Mwinyi lakini mekwenda mbali na kugusa maisha yake ya kimapenzi.
Mchumba wa
Mwinyi, mwanafunzi ambaye hakutaka kumtaja jina kwa sasa, alizisikia skendo za mwandani wake
kupitia kwa marafiki zake na akanuna kwa sababu alikuwa akitaniwa.
Mwinyi
anasema: “Dah! Kwanza kabisa sina mke na sijawahi kuwa na mke kiukweli kabisa,
mimi nina mchumba wangu ambaye ni mwanafunzi na ni mapema kumuweka wazi kwa
sasa.
“Lakini kwa
kifupi, shutuma hizo mchumba wangu zilimshtusha sana, bila kusikiliza utetezi
wangu, alikasirika na kuhuzunika sana, licha ya kutumia muda mwingi kumuaminisha
kwa kumueleza ukweli.
“Kama
unavyojua wanawake wanakuwa na marafiki zao, sasa wanaposikia taarifa kama hizo
juu yangu, alijiona kama namdhalilisha lakini
baada ya kuujua ukweli akakaa kimya na yakamalizika kwa amani.”
Post a Comment