KOCHA msaidizi wa
Simba Mganda, Jackson Mayanja, ametajwa kumrithi aliyekuwa kocha wa Mwadui,
Jamhuri Kihwelu ‘Julio’, aliyetangaza kujiuzulu kufundisha timu hiyo mwishoni
mwa wiki iliyopita.
Katibu wa Mwadui,
Ramadhan Kilao, alisema kwa sasa bado uongozi haujaanza mazungumzo na kocha
yeyote kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Julio, lakini jana walitarajiwa kufanya
kikao cha pamoja ili kujadili suala hilo.
“Julio ameamua
mwenyewe kuachia timu, lakini hakuwa ametoa tamko rasmi na leo jioni (jana),
tutakuwa na kikao naye kwa ajili ya kujua kama anaondoka rasmi ili kuamua ni
kocha gani atachukua nafasi yake.
“Suala la kuanza
mazungumzo na Mayanja si kweli kwani kila mtu anazungumza lake na hatuwezi
kuzungumza na kocha mwingine wakati bado hatujakaa na Julio kujua mustakabali
wake ndani ya timu,” alisema Kilao.
Mayanja ambaye
kwa sasa yupo kwao nchini Uganda, imetajwa kuwa hiyo ni moja ya mipango yake
kwa ajili ya kujiunga na timu hiyo ya Mwadui.
Post a Comment