SIKU moja
baada ya kocha George Lwandamina raia wa Zambia kutua nchini kwa ajili ya
kusaini mkataba wa kuifundisha Yanga, kocha mkuu wa timu hiyo, Hans Pluijm
ameandika barua ya kujiuzulu nafasi hiyo kuanzia leo.
Habari za
kubadilishwa kwa benchi la ufundi la Yanga zilikuwepo kwa zaidi ya wiki sasa na
Pluijm hakupewa taarifa yoyote hata pale alipowasili Mzambia huyo hapo jana
bado uongozi wa Yanga ulisisitiza kuwa ni mwajiriwa wao halali.
Habari za
uhakika ambazo BOIPLUS imezipata ni
kwamba Pluijm hajafurahishwa na maamuzi ya viongozi wa Yanga kumleta mbadala
wake pasipo kumpa taarifa zozote huku yeye wakiendelea kumwambia kuwa bado ni
kocha wao.
Pluijm
amepanga kuwaaga wachezaji wake kesho kwenye mazoezi ya asbuhi na kueleza kuwa
Yanga italazimika kumlipa kocha huyo mshahara wa mwezi mmoja huku tayari
zikiwepo taarifa za kwamba Lwandamina angesaini mkataba wa miaka miwili muda
wowote kuanzia leo.
Maamuzi hayo
yatakuwa magumu kwa timu ya Yanga ambayo keshokutwa inakabiliwa na mechi dhidi
ya Ruvu Shooting itakayochezwa Uwanja wa Uhuru ikiwa imetoka kuifunga Kagera
Sugar bao 6-2 na kukusanya pointi 21 ilishika nafasi ya pili.
Post a Comment