SIMBA leo
imeendelea kujiimarisha kileleni mwa ligi kuu baada ya leo kuicharaza bila
huruma Toto African ya Mwanza mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Uhurujijini Dar.
Kwa matokeo
ya leo Simba inaendelea kukaa kileleni ikiwa na alama 29 baada ya kushuka
uwanjani mara 11.
Simba ambayo
ilionekana tangu awali inanjaa ya mabao iliaandika bao lake la kwanza dakika ya 43 kupitia kwa Mzamiru Yassin
aliyeunganisha vyema krosi ya Blagnon.
Kipindi cha
pili Simba walirudi kwa kasi ileile kama ya kipindi cha kwanza na kufanikiwa kuandika
bao la pili kupitia kwa Laudit Mavugo aliyeingia dakika ya 49 na yeye kutrupia
dakika ya 52 akiunga krosi ya Mohamed Ibrahim ambaye alifanya kazi ya zida
kumpita mlinzi wa Toto na kupiga shuti lililotinga wavuni moja kwa moja.
Wakati wengi
wakidhani mpira ungeisha kwa SImba kushinda mabao 2-0, Mzamiru aliiondoa fikra
hiyo kwani dakika ya 74 aliukwamisha mpira tena wavuyni akiunganisha mpira wa
kona uliopigwa na Kichuya, ambapo ulitua mguuni kwa ‘muuaji’ huyo na kutandika
shuti ndani ya 18.
Mechi nyingi
iliwakutanisha Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine ambapo wenyeji walibanwa na
kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Mbao. Goli
la Prisons lilifungwa na Sibianka dakika ya 90 kwa njia ya penalty huku Boniface
Maganga akiifungia Mbao dakika ya 84.
Post a Comment