WAKATI mashabiki na wanachama kadhaa
wa Yanga wakilalama kuondokewa na kocha wao kipenzi, Hans van Pluijm, uongozi
wa klabu hiyo unakamilisha taratibu za kuingia mkataba na Mtendaji Mkuu mpya wa
klabu hiyo Mfaransa, Jerome Dufourg, ambaye rekodi yake inatisha.
Mtendaji huyo mpya pindi
atakapoajiriwa atakuwa na mamlaka ya juu kabisa katika mambo yote ya uendeshaji
wa klabu, ambapo taarifa za ndani ambazo tumezipata zinadai kuwa yuko karibu
kusaini mkataba wa miaka mitatu.
Dufourg, raia wa Ufaransa, ni miongoni
mwa watu wanaotambulika na Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA) kutokana na
kuwa na wasifu (CV) wa juu katika mambo ya soka.
Mfaransa huyo kijana mwenye umri wa
miaka 30, ana shahada ya juu ya Fifa katika uongozi wa soka kuhusiana na uchumi
pamoja na utawala.
Katika nchi za Afrika, amewahi kufanya
kazi Shirikisho la Soka nchini Rwanda
(FERWAFA) pamoja na klabu ya FC Talanta ya Ligi Daraja la Pili nchini
Kenya.
DIMBA
Post a Comment