Baraza la
michezo la Taifa BMT limeagiza michakato yote inayoendelea ya kubadilisha
umiliki wa timu kutoka kwa wanachama kwenda kwenye umiliki wa hisa na
ukodishwaji kwa vilabu vyote vya michezo usitishwe mara moja hadi hapo
marekebisho ya katiba zao kwa mujibu wa sheria ya Baraza la michezo la taifa na
kanuni za msajili.
Akiongea
mbele ya waandishi wa Habari leo hii katibu mkuu wa BMT,Mohamed Kiganja amesema
kwamba baraza linapenda kuona kwamba wahusika wakuu wa jambo hilo hasa klabu za
Simba na Yanga wanafuata sheria na taratibu za nchi katika kufikia malengo yao.
Amesema
kwamba endapo vilabu hivyo kama vitaendelea na mchakato huo kabla ya taratibu
za kurekebisha katiba zao kisheria ni kosa na hatua stahiki zitachukuliwa dhidi
ya watakaokiuka maelezo hayo.
"Hivi
karibuni imeibuka michakato ya watu wakitaka kubadilisha umiliki wa vilabu vya
wanachama na kuvielekeza kwenye utaratibu wa hisa na ukodishwaji,vitendo hivi
vimesababisha migogoro mikubwa ambayo inaashiria uvunjifu wa amani ndani ya
tasnia ya michezo kwani imefikia hatua watu wanaenda mahakamani mfano mzuri
ndani ya klabu ya Yanga"alisema Kiganja.
Ameongeza
kuwa makundi ya wapenzi na wanachama wamejikita katika mijadala ambayo hatma
yake ni kuzidi kuibomoa jamii badala ya kuijenga na kuimalisha michezo nchini.
Post a Comment