April 10, 2025 04:05:51 AM Menu




WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh.Mwigulu Nchemba amemrejesha Kocha wa Yanga Hans Van De Pluijm ambaye alijiuzulu kuiongoza timu hiyo mapema wiki hii.
Pluijm alichukua hatua hiyo baada ya kupata taarifa kuwa Yanga imemleta Kocha George Lwandamina ili achukue nafasi yake.
Katika mazungumzo yaliyodumu takribani siku tatu, mchana huu Mwigulu Nchemba amefanikiwa kumrejesha kocha huyo ndani ya viunga vya jangwani na tayari kwa kuendelea na kazi yake ya Ukocha.
 Hii ni mara ya pili Mwigulu Nchemba anafanikiwa kuweka mambo sawa ndani ya Klabu ya ya Yanga, msimu uliopita alifanikiwa kumrejesha Kiungo Haruna Niyonzima kuichezea Yanga.
Ikumbukwe, Mwigulu Nchemba ni mdau wa michezo nchi na mpenzi wa soka na mwanachama wa Jangwani.
28 Oct 2016

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top