STRAIKA
ghali zaidi kwenye kikosi cha Yanga, Obrey Chirwa aliyetua katika timu hiyo kwa
dau linalotajwa kuwa zaidi ya sh milioni 200 ameendelea kulipa deni kidogkidogo
baada ya leo kuifungia mabao mawili klabu yake hiyo kwenye mchezo wa ligi kuu
dhidi ya Kagera Sugar ya mkoani Bukoba na Jangwani kuibuka na ushindi wa mabao 6-2.
Chirwa
aliyetua Yanga mwaka huu akitokea FC Platinum ya Zimbabwe alikuwa akilalamikiwa
vikali na mashabiki wa timu hiyo kutokana na kutofunga mabao kuanzia kwenye
michuano ya Kombe la Shirikisho na mechi za awali za ligi kuu kabla ya ‘kuona
mwezi’ katika mchezo dhidi ya Mtibwa uliopigwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar.
Kagera
wakiwa kwenye dimba lake la nyumbani la Kaitaba, walikuwa wa kwanza kupata bao
katika dakika ya kwanza ya mchezo kupitia kwa Baraka Ramadhani aliyepiga shuti kali nje ya 18 na kumbabatiza
beki wa Yanga, Dante na hivyo kumchanganya kipa Deo Munish ‘Dida’.
Baada ya bao
hilo kuingia, Yanga waliliandama lango la Kagera na kufanikiwa kusawazisha
dakika ya tatu mfungaji akiwa ni Donald Ngoma. Baada ya bao hilo kuingi, Yanga
waliendelea kulisakakama lango la wapinzani wao hao ambapo dakika ya tano Simon
Msuva alifanikiwa kufungwa bao akimalizia mpira uliotemwa na kipa Cassillas.
Obrey Chirwa
alifunga bao la tatu kwa Yanga naye pia akiumalizia mpira uliotemwa na
Cassillas baada ya mchezaji wa Yanga kupiga shuti kali ambalo alishindwa
kulidaka na hivyo mpira kumponyoka. Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa Yanga
kuwa mbele kwa mabao 3-1.
Kipindi cha
pili timu zote zilirudi zikiwa moto ambapo Kagera Sugar walifanikiwa kuandika
bao la pili mfungaji akiwa ni yuleyule Baraka katika dakika ya 48 akimalizia
mpira uliokuwa ukiambaa langoni kwa Yanga. http://spotiripota.blogspot.com/2016/10/chirwa-apiga-mbili-yanga-ikiiua-kagera.html
Mabao
mengine ya Yanga yalifungwa na Deus Kaseke dakika ya 57, Obrey Chirwa (63) na
Donald Ngoma dakika ya 72. Chirwa ambaye
awali alikuwa na mabao mawili ukichanganya na ya leo jumla yanakuwa manne. http://spotiripota.blogspot.com/2016/10/chirwa-apiga-mbili-yanga-ikiiua-kagera.html
Post a Comment