MWENYEKITI wa
Kamati ya usajaili ya Simba, Hans Poppe ameunga mkono kuwa ni kweli nahodha wa
timu hiyo Jonas Mkude anaweza kuwa hajakomaa katika kuwaongoza wenzake ndani ya
uwanja.
Mkude ambaye ni
zao la klabu hiyo, wikiendi iliyopita alipata kadi nyekundu ya moja kwa moja na
mwamuzi Martin Saanya kwa madai kuwa alimsukuma hadi akaanguka kwenye mchezo wa
ligi dhidi ya Yanga ambao uliisha kwa sare ya bao 1-1.
Akizungumza Hans
Poppe kuhusiana na kadi nyekundu aliyopewa kiungo huyo kuonyesha kuwa hajakomaa
katika suala la kuwaongoza wenzake hasa linapotokea tatizo uwanjani alisema:
“Ni kweli, Mkude
hakuwa sahihi, yeye ndiye angesimama na kuwatuliza wenzake. Kama tungebaki kumi
na moja sidhani kama Yanga wangesimama.”
Post a Comment