SIMBA ipo
kileleni mwa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 26 katika mechi 10, klabu hiyo
imedai endapo mastraika wake Ibrahimu Ajibu na Laudit Mavugo wakitulia na
kuelewana basi ubingwa wao mapema.
Kocha Msaidizi
wa Simba, Jackson Mayanja alisema, wawili hao bado ‘combination’ yao
haijaelewana uwanjani hivyo wanashindwa kupata mabao mengi.
“Mpaka
mchezaji anapata nafasi ya kuanza kwenye kikosi ina maana amepewa majukumu ya
kuisaidia timu kutokana na uwezo wake na maelewano ya wenzake uwanjani.
“Sasa Ajibu
na Mavugo wanapokuwa mazoezini wanafanya vizuri na tunawapa nafasi ya kuanza
pamoja lakini tunashindwa kuelewa inakuwaje katika katika mechi hawaelewani.
“Bado
tunalifanyia kazi tatizo hilo kwani tunahitaji ubingwa, Ajibu na Mavugo wakielewana
tu basi tutapata mabao mengi na kuwa na uhakika wa ushindi na hapo tutatangaza
ubingwa mapema tu,” alisema Mayanja raia wa Uganda.
Pamoja na
hayo, kwa mujibu wa takwimu za mechi 10 za Simba ilizocheza mpaka sasa,
washambuliaji hao kila mmoja amefunga mabao matatu.
Katika mechi
tisa Ajibu alizocheza sambamba na Mavugo, amefanikiwa kumpa mshambuliaji huyo
asisti ya bao moja walipoifunga Ruvu Shooting mabao 2-0, Mavugo hajafanikiwa
kutoa asisti yoyote kwa pacha wake huyo.
Post a Comment