TARATIBU Yanga
imeanza kupungua makali yake kulinganisha na misimu miwili iliyopita ya Ligi
Kuu Bara, sasa kocha wa timu hiyo, Hans vanDerPluijm amekiri kuna tatizo kwenye
kikosi chake cha sasa katika mbio za kutetea ubingwa.
Yanga ipo nafasi
ya tano katika ligi ikiwa na pointi 11, sita nyuma ya vinara Simba lakini
yenyewe ina mchezo mmoja mkononi dhidi ya JKT Ruvu uliopangwa kuchezwa katikati
ya mwezi huu.
Hadi sasa Yanga
ina mabao tisa wakati Simba inayo 13, imefungwa mabao mawili wakati Wekundu wa
Msimbazi wamefungwa matatu.
Licha ya Pluijm
kusita kubainisha ni safu gani yenye matatizo, lakini Championi Jumamosi
linafahamu kocha huyo anaumiza kichwa na safu yake ya ushambuliaji na ile ya ulinzi.
Pluijm alisema:
“Ni kweli kuna tatizo kwenye kikosi changu, lakini kama kocha mwenye weledi si
jambo jema kuelezea kila kitu kwenye vyombo vya habari.
“Ni masuala ya
mimi kama kocha kuangalia jinsi gani nayafanyia kazi matatizo hayo, lakini kweli
makosa yapo na kila baada ya mechi lazima nichukue jukumu la kuangalia njia
sahihi za kuyatatua.”
Katika mabao tisa
ya Yanga, ni AmissiTambwe tu aliyeonyesha uhai wa kufunga kati ya mastraika wa
timu hiyo kwani Donald Ngoma amefunga bao moja tu wakati MalimiBusungu, Obrey
Chirwa na Matheo Anthony hakuna aliyefunga.
Badala yake, winga
DeusKaseke ana mabao mawili, Simon Msuva na Juma Mahadhi wana mojamoja.
Post a Comment