Shirikisho
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linaalika umma kuwania zabuni ya kubuni
mwonekano mpya wa jezi mpya za timu ya taifa zitakazotumika kwa msimu wa
2017/18 na msimu wa 2018/19.
Kwa
taarifa hii, TFF imefungua milango kwa umma ambako mtu mmoja mmoja anaweza
kuwasilisha ubunifu wa mwonekano wa jezi hizo katika ofisi zake zilizoko Uwanja
wa Kumbukumbu ya Karume ulioko kwenye makutano ya barabara za Uhuru na
Shaurimoyo, Ilala jijini Dar es Salaam.
Wakati
mwisho wa kupokea zabuni hizo ni Novemba 30, 2016, sharti kwa mbunifu ni
kutoiga ubunifu kutoka makampuni makubwa ya vifaa vya michezo. Na Mbunifu Bora
au Mshindi wa jezi ambazo zitakuwa lazima ziwe na nembo ya TFF na Bendera ya
Taifa, atazawadiwa shilingi milioni mbili (Sh milioni 2).
Jezi za sasa za
Timu ya Taifa ni rangi ya bluu kwa michezo nyumbani na nyeupe mechi za ugenini.
Post a Comment