KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans pluijm amesema mchezo wao wa leo dhidi
ya Toto utakaopigwa Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, utakuwa mgumu lakini anaamini
vijana wake watapigana na kuondoka na alama tatu ugenini.
“Utakuwa mchezo mgumu kwa pande zote, kwani kila mmoja atataka
matokeo mazuri, lakini niwahakikishie mashabiki wetu kuwa, tumejiandaa vizuri
na malengo yetu ni kuondoka na pointi zote tatu,” alisema.
Msimu uliopita timu hizi zilipokutana Yanga waliibuka kidedea,
wakiwafunga Toto African mabao 4-1 mchezo wa mzunguko wa kwanza, uliochezwa
Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam na kuibuka na ushindi mwingine wa mabao
2-1 Uwanja wa CCM Kirumba.
Habari njema kwa Wanayanga katika mchezo wa leo ni kwamba, huenda
mshambuliaji wao mwenye bahati ya kucheka na nyavu, Amis Tambwe, akacheza baada
ya kupata nafuu kutokana na majeraha yaliyokuwa yakimkabili aliyoyapata kwenye
mchezo dhidi ya Azam FC.
Katika mchezo huo Yanga itawakosa wachezaji wake watatu; Juma
Abdul, Andrew Vincent ‘Dante’, Malimi Busungu pamoja na kipa Ally Mustafa
‘Barthez’ ambao ni majeruhi, lakini haitakuwa na madhara yoyote, kwani kikosi
hicho kimesheheni wachezaji wazuri.
Post a Comment