Kocha mkuu wa Yanga, Mholanzi Hans Pluijm amemchimba mkwara mzito nyota wa kikosi hicho Haruna Niyonzima akimtaka kuhakikisha anapandisha kiwango chake la sivyo ataozea benchi.

Niyonzima raia  wa Rwanda amekuwa hapati nafasi ya kucheza mara kwa mara tangu msimu uanze hali iliyowafanya mashabiki wa Yanga kujiuliza kuna nini.

“Mwalimu (Pluijm) amesisitiza kwamba Niyonzima apandishe kiwango na kufuata mfumo wake la sivyo atakuwa kwenye wakati mgumu kupata nafasi kikosini,” kilisema chanzo hicho.

Kwa upande wake, Niyonzima alisema matatizo ya kifamilia aliyonayo yamemfanya kushindwa kufanya kazi yake kwa ufanisi mkubwa na kusababisha kushindwa kuonekana uwanjani.

“Nilikuwa nina matatizo makubwa sana ya kifamilia ndio maana umeona nimeshindwa kufanya vizuri, akili ilikuwa haiko sawa kwa kweli. Ila nashukuru nimeyapunguza baadhi,” alisema Niyonzima.

Kiungo huyo aliongeza kuwa hakuna tatizo lingine linalomkabili zaidi ya matatizo ya kifamilia na kuwaahidi wapenzi wa Yanga kukaa mkao wa kula na kupata vitu vizuri kutoka kwake.

“Mambo yatakuwa mazuri wasiwe na wasiwasi, mimi nipo sana tu Yanga sina tatizo na mtu yeyote wasubiri waone kazi,” alisema Niyonzima.

Niyonzima aliingia dakika za mwisho kwenye mchezo kati ya Yanga na Stand United na ule dhidi ya Simba uliopigwa Oktoba mosi Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

 
Top