April 10, 2025 11:08:29 PM Menu






RIPOTI ya Daktari wa Simba, Yassin Gembe inasema kuwa hali ya straika wa kikosi hicho, Fredrick Blagnon raia wa Ivory Coast inaendelea vizuri lakini atatakiwa kuwa nje ya muda wa siku saba akiuguza jereha alilolipata jana Jumapili.

Blagnon aliumia kwenye mchezo wa ligi kuu Jumapili katika Uwanja wa Taifa wakati Simba ikivaana na Toto African ya Mwanza. Katika mchezo huo Simba ilishinda mabao 3-0 huku Blagnon akitoa asisti ya bao la kwanza lililofungwa na Mzamiru Yassin.
Straika huyo aliumia usoni karibu na jicho na kusababisha damu kumtoka kabla ya kutolewa na kwenda kufanyiwa matitabu ambapo alishonwa nyuzi nne.
Gembe amesema Blagnon atafanya mazoezi baada ya siku tatu chini ya uangalizi maalum kabla ya kujinga na wenzake pindi hali yake itakapoimarika.
24 Oct 2016

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top