STRAIKA wa
Yanga, Obrey Chirwa, amempoteza vibaya, Laudit Mavugo, baada ya kucheza mechi
chache na kuweza kumkimbiza straika huyo wa Burundi.
Chirwa
alianza kutoa ‘gundu’ kwa kufunga bao lake la kwanza tangu atue kuichezea timu
hiyo kwenye ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa.
Mzambia huyo
aliyetua kuichezea Yanga kwa dau la Sh milioni 200, amecheza mechi za Kombe la
Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe, Medeama na Mo Bejaia na mechi za ligi,
huku nyingine ya kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar bila kufunga bao lolote.
Lakini sasa kwenye
michezo tisa waliyocheza Yanga huku Chirwa akicheza mechi tano amefanikiwa
kufunga mabao mawili na kuweza kumkimbiza Mavugo ambaye naye kwa sasa ana ukame
wa mabao.
Kwa upande
wake Mavugo ambaye timu yake imecheza michezo 10, huku akipewa nafasi ya kuanza
kwenye kikosi hicho mara tisa akikosa mchezo mmoja pekee dhidi ya Mbeya City,
ameweza kufunga mabao matatu mpaka sasa.
Mavugo
ambaye mara nyingi amekuwa akitoka kipindi cha pili na kumpisha Fredrick
Blagnon, kwa sasa ameshindwa kufunga kwenye mechi za mfululizo za timu hiyo.
Post a Comment