Yanga na
Simba jana zilicheza mchezo wa 83 kwenye ligi kuu bara tangu mwaka 1965
ilipoanzishwa Ligi ya Taifa na sasa ligi kuu na aliyekuwa Kocha wa Taifa Stars,
Milan Celebic.
Katika
mchezo wa jana timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1. Bao la Yanga lilifungwa na
Amissi Tambwe huku Simba wakisawazisha kupitia kwa Shiza Kichuya.
Katika
kipindi chote hicho, msisimko wa kuelekea mechi hizi umekuwa mkubwa, bila
kujali nani anawania kitu gani na yupo katika kiwango kipi.
Msimu
uliopita Simba haikuambulia kitu kwa Yanga kwani ilifungwa mechi mbili zote
tena kwa idadi ya mabao 2-0 kwenye kila mchezo. Sasa katika mechi 13 za mwisho
ambazo zimewakutanisha mahasimu hawa wa soka nchini, Kocha Goran Kopunovic wa
Simba ndiye kocha wa mwisho kuifunga Yanga.
Kopunovic
aliiongoza Simba kuifunga Yanga Machi 8, 2015 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam ambapo Simba ilishinda bao 1-0. Bao hilo pekee la Simba lilifungwa na
Emmanuel Okwi dakika ya 53.
Ikumbukwe ya
kuwa, Okwi raia wa Uganda alikuwa amerejea Simba baada ya kuwa katika mgogoro
na Yanga aliyokuwa akiichezea siku za nyuma.
Licha ya
kuifunga Yanga Machi 8, Simba iliachana na Kopunovic Mei 17, 2015 kwa kile
kilichoelezwa kuwa haikuwa tayari kuongeza mkataba mpya na kocha huyo aliyetaka
alipwe mshahara wa dola 9000 (Sh milioni 19.2) na kupewa fedha za kusaini
mkataba mpya dola 50,000 sawa na Sh milioni 106.8.
Baada ya
Kopunovic alipoondoka Simba ikampa kazi Dylan Kerr raia wa Uingereza ambaye
naye alimuachia timu Jackson Mayanja wa Uganda ambaye sasa anamsaidia Joseph
Omog wa Cameroon.
Post a Comment