KITENDO cha nahodha na kiungo wa Simba SC, Jonas
Mkude kupewa kadi nyekundu (Red), katika mechi yao ya mwisho dhidi ya Yanga SC
kimeitikisa timu hiyo kuelekea katika michezo yao inayofuata.
Mkude alipewa kadi hiyo akidaiwa kumsukuma
mwamuzi mara baada ya Amissi Tambwe wa Yanga kufunga bao la kuongoza.
Benchi la ufundi la Simba chini ya Mcameroon,
Joseph Omog limekiri kuwa na kazi ngumu ya kuziba nafasi ya kiungo mkabaji
katika kikosi hicho kwa kumkosa Mkude hasa ukizingatia wana mechi ngumu mbele
yao dhidi ya Prisons na Mbeya City mkoani Mbeya.
Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja
alifafanua kuwa ingawa kikosi chao ni kipana na kina wachezaji wengi lakini
bado mchango wa Mkude utaendelea kukosekana kutokana na staili yake ya
uchezaji.
“Ndiyo tuna kikosi kipana na wachezaji wazuri
lakini bado tuta-miss mchango wa Mkude akiwa uwanjani, inafahamika umuhimu
wake. Katika nafasi yake anaweza kucheza Mzamiru (Yassin), Awadh Juma na
wengine lakini bado tutaangalia nani atafiti vizuri katika mazoezi ya
maandalizi.
“Sitaki kuizungumzia ile kadi aliyopewa maana
mwamuzi ana maamuzi yake lakini kivyovyote katika timu lazima itakuwa
imegharimu,” alisema Mayanja, raia wa Uganda.
Post a Comment