WINGA wa zamani wa Yanga,
Mrisho Ngassa, anayekipiga Fanja ya nchini Oman yupo Bongo kwa sasa na inadaiwa
kuwa amekuja kwa ajili ya kufanya mazungumzo na uongozi wa Yanga ili kujaribu kuushawishi
uweze kumsajili.
Hata hivyo, habari za kuaminika
kutoka ndani ya Yanga zimedai kuwa nyota huyo ambaye pia amewahi kuzitumikia Kagera
Sugar, Simba, Azam na FreeState ya Afrika Kusini, ameondoka kwa kudanganya
katika timu yake ya Fanja na kuja hapa nchini ili kufanikisha dili hilo.
Mara kadhaa Ngassa amekuwa
akihusishwa kutaka kurejea kikosini humo tangu aachane nacho kwenda FreeState
baada ya msimu wa 2014/15.
“Ni kweli Ngassa yupo hapa
nchini na hivi karibuni alikutana na baadhi ya viongozi wetu na kuzungumza nao
akiwaambia kuwa anataka kurejea Yanga.
“Katika timu yake hiyo ya
Fanja aliaga kuwa ana matatizo ya kifamilia, hivyo anatakiwa akayamalize, nao
bila ya kujua wakamruhusu kumbe lengo lake kubwa ni kuja kuushawishi uongozi
ili uweze kumsajili katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili.
“Hata hivyo, mpaka sasa
viongozi wametofautiana kuhusiana na suala hilo ambapo wapo wanaotaka na wengi
hawataki wanadai kuwa kwa sasa hana sifa za kuitumikia Yanga,” kilisema chanzo
hicho cha habari.
Alipotafutwa Ngassa kuhusiana
na ishu hiyo, alikiri kuwepo nchini kutokana na matatizo ya kifamilia
yaliyosababisha aje ili kuyatatua.
“Mkataba wangu haunibani
kujiunga na klabu yoyote baada ya miezi mitatu, muhimu ni utaratibu wa
kiusajili kufuatwa,” alisema na kufunguka zaidi kuhusu Yanga:
“Yanga ni timu yangu ya
zamani na sioni sababu ya kutorejea kutokana na mafanikio niliyoyapata nikiwa
pale.”
Post a Comment