AJIB NA JUUKO

BEKI wa zamani wa Simba, Miraj Adam, amelitahadharisha benchi la ufundi la timu hiyo kwa kulitaka kuhakikisha linampanga beki wa kati, Mganda, Juuko Murshid kama wanataka ushindi kwenye mchezo wao dhidi ya Yanga.
Simba na Yanga zitashuka dimbani leo kuumana katika pambano la Ligi Kuu Bara, litakalopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Miraj amesema kuwa ili Simba ijihakikishie usalama wake katika eneo la ulinzi, inapaswa kumpanga Murshid, kwani kinyume cha hapo watakuwa na wakati mgumu kutoka kwa washambuliaji wa Yanga.
Alisema anaamini mchezo huo utakuwa na presha, hivyo wana kila sababu ya kumtumia Murshid kutokana na uzoefu alionao katika Ligi Kuu.
“Lufunga ni beki mzuri, lakini tatizo lake anacheza soka ya upole, unajua wale akina Tambwe na Ngoma wanahitaji kukabwa na mabeki wakorofi wababe ili kuweza kuwapunguza kasi yao,” alisema Adam.
Adam, ambaye kwa sasa anakipiga African Lyon, inayoshiriki Ligi Kuu Bara kwa kuangalia uzoefu, anawapa nafasi kubwa Yanga kushinda mchezo huo kuliko Simba, ambayo ina wachezaji wengi wageni.
“Mimi nawapa nafasi kubwa Yanga kushinda, wapo vizuri kila idara, tofauti na Simba, lakini cha muhimu leo Simba watake wasitake, lazima Murshid wampange, vinginevyo hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwao,” alisisitiza Miraj.
Murshid amekuwa hana nafasi ya kuanza katika kikosi cha Simba, baada ya klabu hiyo kumsajili beki Method Mwanjali kutoka Zimbabwe.

Post a Comment

 
Top