Malipo ya mishahara kwa mwezi ya wachezaji, benchi la ufundi na sekretarieti kwa Yanga jumla ni shilingi milioni 160, hii ni kwa mujibu wa tamko alilolitoa mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji wakati wa uchaguzi mkuu wa timu hiyo Juni 11, mwaka huu.
Chanzo kimoja cha habari ndani ya Yanga kimeliambia gazeti hili kuwa katika kiasi hicho, kitita cha Sh milioni 120 hutolewa kila mwezi kwa ajili ya kuwalipa wachezaji tu na kinachobaki ndiyo wanagawana wengine.
Kwa upande wa Simba, malipo ya mishahara ya wachezaji, benchi la ufundi pamoja na sekretarieti ni Sh milioni 78 tu kwa mwezi, hiyo ni kwa mujibu wa chanzo chetu cha ndani ya Simba.

Ukilinganisha hapo utakuta Simba imefunikwa na Yanga kwa jumla ya kitita cha Sh milioni 82, yaani kila mwezi Yanga inatoa Sh milioni 82 zaidi ya kiasi inachotoa Simba.

Post a Comment

 
Top