NYOTA watatu wa kikosi cha kwanza cha
Yanga, Donald Ngoma, Thaban Kamusoko na Nadir Haroub ‘Cannavaro’, wameshindwa
kufanya mazoezi kutokana na sababu tofauti.
Katika mazoezi ya timu hiyo
yaliyofanyika jana katika Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini, jijini Dar es
Salaam, blog hii ilishuhudia wachezaji hao wakiwa nje ya dimba, huku wakiwa
wamevalia mavazi ya kawaida.
Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, alisema
jana kuwa, wachezaji hao hawakufanya mazoezi na wenzao kutokana na sababu
mbili, ruhusa maalumu na majeraha.
“Bossou yupo katika kikosi cha timu ya
taifa ya Togo, lakini Niyonzima, Malimi Busungu na Beno Kakolanya wana ruhusa
maalumu ya kuwa na matatizo ya kifamilia,” alisema Hafidh.
Licha ya kuwakosa nyota hao, Yanga
iliendelea na mazoezi yake kama kawaida na leo inatarajia kuhamia katika fukwe
za Gymkhana, Posta, jijini humo kujiwinda na mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting,
utakaopigwa Alhamisi ya wiki ijayo.
Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der
Pluijm, ameanza kusuka safu yake ya ulinzi kwa kutengeneza safu mpya,
ikimjumlisha Pato Ngonyani, Kelvin Yondani na Andrew Vicent ‘Dante’ kwavile
atamkosa Bossou, ambaye anaitumikia Togo.
Post a Comment