BAADA ya
safari ndefu ya saa kadhaa, kikosi cha Mbeya City FC tayari kimewasili jijini
Mbeya kujiwinda na mchezo ujao wa ligi
kuu soka Tanzania bara dhidi ya Azam Fc
uliopangwa kuchezwa mwishoni mwa juma hili kwenye uwanja wa Sokoine.
Muda
mfupi uliopita meneja wa kikosi hiki
Geoffrey Katepa ameimbia mbeyacityfc.com kuwa Mwalimu Kinnah Phiri ameamua
kuwapa mapumziko ya siku moja wachezaji wake ili waweze kupumzika kutokana na
uchovu wa safari ndefu na siku ya kesho jioni wataingia kwenye uwanja wa Sokoine kuanza mazoezi ya matayarisho ya mchezo huo
wa jumamosi.
“Mwalimu
ametoa mapumziko siku ya leo hii ni kwa sababu tumekuwa na safari ndefu kutoka
Mwanza tukipitia Tabora, hivyo mazoezi ya matayarisho ya mchezo ujao yataanza
kesho jioni.
“Jambo muhimu
ni kwamba tunamshukuru Mungu kwa
kutuwezesha kupata matokeo mazuri kwenye michezo yetu mitatu ya mwanzo wa
msimu,hili limetufanya kuongoza ligi kwa mara ya kwanza, jambo ambalo pia
limetuongezea morali kubwa ya kushinda dhidi ya Azam FC Jumamosi” alisema.
Akiendelea zaidi Meneja Katepa alisema kuwa kitengo cha
utabibu cha City kinachoongozwa na Dr Joshua Kaseko kimesibitisha kuwa wachezaji wote wako kwenye hali nzuri kwa
maana ya hakuna aliye majeruhi na baada
ya mapumziko ya leo wote watakuwa tayari kwa mazoezi ya kujiandaa kucheza
mchezo wa jumamosi.
“Jopo la
madaktari wetu wamenithibitishia kuwa kikosini
hakuna mchezaji mwenye majeraha, wote wana hali nzuri hivyo baada ya kupisha mapumziko ya leo wote
watakuwa tayari kwa mazoezi ya matayarisho ya mchezo”. alimaliza.
Kwenye
michezo mitatu iliyopita City ilifanikuwa kuibuka na pointi saba, kufuatia
suluhu ya bila kufungana na Kagera Sugar na baadae kuiadhibu Toto Africans bao
1-0 na mwisho kuhitimisha kwa kuifunga Mbao Fc
bao 4-1 na kushika usukuni wa ligi kuu.
Post a Comment