MKUU wa
Kitengo cha Masoko na Biashara TSN, Jahu Mohammed Kessy akiwakabidhi wasanii
jezi kwa ajili ya mechi ya kuchangia maafaa ya tetemeko la ardhi Bukoba
Kampuni ya
TSN Kwa kushirikiana na Wasanii wa bongo
fleva na bongo Movie wamejitokeza kuwezesha mechi maalum kuchangia wahanga wa
Tetemeko la Ardhi lililotokea Bukoba mkoani Kagera.
Mkuu wa
Kitengo cha Masoko na Biashara Jahu Mohamed Kessy, amesema TSN imejitokeza
kudhamini mechi hiyo itayofanyika Uwanja wa Taifa, keshokutwa Jumapili ambapo
amewataka wananchi, mashirika na kampuni mengine binafsi kujitokeza kwa wingi
kwa ajili ya kuchangia na kuwezesha misaada kwa wananchi wa Kagera waliopata
maafa kutokana na tetemeko hilo la ardhi.
Alisema wao
kama TSN wameguswa na janga hili na hivyo mbali na michango yao mingine ya moja
kwa moja wameona umuhimu wa kushirikiana na wasanii wa Bongo Fleva na Bongo
Movie kuhamasisha uchangiaji huo kwa pamoja ilikuweza kuwashirikisha na
wengine.
“TSN,
Tanzania sisi nyumbani, tunaunganisha nguvu ya wasanii hawa kutoka katika
tasnia hizi mbili tofauti kwa lengo la
kuhamashisha uchangiaji wa pamoja,”
Post a Comment