KIUNGO wa
zamani wa Man United, Paul Scholes amewatupia lawama baadhi ya wachezaji baada
ya Manchester United kupoteza mchezo dhidi ya Watford kwa mabao 3-1.
Scholes,
ambaye anafanya kazi ya uchambuzi katika kituo cha runinga cha BT Sport, amedai
kwamba licha ya uwepo wa majina makubwa uwanjani lakini United walionekana
kucheza chini ya kiwango.
“Nadhani kwa
uwezo uliooneshwa na mchezaji mmoja-mmoja uwanjani haukuwa wa kuridhisha.
kwenye upande wa umiliki wa mpira ndiyo kabisa ovyo, kila mara walikuwa
wakipoteza mpira.”
Moja ya
wachezaji ambao Scholes amewatupia lawama sana ni Marouane Fellaini kwa namna
alivyocheza kwenye eneo lake la kiungo.
“Yeah kweli
nadhani Fellaini alijitahidi kwa kadri ya uwezo wake; alifanya kazi yake
alivyoweza,” alisema Scholes.
“Lakini kama
wewe ni mtu wa Manchester United, unahitaji kuona zaidi ya alivyocheza.
“Unahitaji
mtu ambaye anaweza kuzuia mashambulizi na kucheza mpira pia, mtu ambaye anaweza
kudhibiti wapinzani lakini anaweza kuweka timu mabegani mwake, kusukuma timu
mbele na kupiga pasi za maana kuelekea goli la wapinzani.
“Sijui
kwanini Michael Carrick yupo pale halafu hachezeshwi. Awali alionekana kama
anaondoka hivi lakini amebaki halafu hachezeshwi. Hata sijui nini kimempata.”
Post a Comment