MKATABA wa beki wa Azam, Pascal Serge Wawa, na klabu yake unakaribia kumalizika na kuna tetesi kuwa staa huyo wa kimataifa wa Ivory Coast, ananukia kwenye kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga.

Hivi karibuni, Wawa aliwahi kunukuliwa na mtandao mmoja wa michezo nchini akisema kuwa,licha ya mkataba wake Azam kubakisha miezi miwili, hafahamu juu ya mustakabali wake ndani ya timu hiyo.

Wawa alisemabado hajaanza mazungumzo yoyote ya kuongeza mkataba nauongozi wa klabu yake hiyo na kufunguka kuwa kwa sasa kuna klabu tatu zinaitaka saini yake, ambapo alidai kuwa mbili ni kutoka Uarabuni huku moja ikiwa ni ya hapahapa nchini.
Licha ya kutoweka wazi ni timu gani ya hapa iliyopeleka ofa kwake,Spotiripota tunataarifa kuwa ofa hiyo inatoka Yanga kwa sababu miamba hiyo ya Jangwani ndiyo klabu pekee nchini ambayo inaweza kuwa na nguvu ya fedha ya kupambana na Azam.
 Mchezaji huyo ambaye kwa sasa anasugua benchi kwa muda mrefu sasa kutokana na majeraha ya goti aliyopata Aprili 10, mwaka huu wakati timu hiyo ikiichapa Esperance ya Tunisia kwa mabao 2-1 kwenye mchezo wa raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam, Saad Kawemba, hakutaka kuweka wazi kama klabu hiyo ina mpango wa kumbakisha beki huyo au la, kitu ambacho bosi huyo hakutaka kukiweka wazi.
 Kawemba alisema suala la mazungumzo ya kuongeza mkataba lipo kati ya klabu ya mchezaji husika na si lazima kutangaza kuwa ni lini watakaa na kuzungumza.
“Mbali na Wawa, wapo wachezaji takribani sita ambao mikataba yao imemalizika na wote hao wapo kwenye kikosi cha kwanza, hivyo lini uongozi utafanya mazungumzo nao kwa ajili ya mkataba mpya ni siri yetu na si lazima tuweke wazi,” alisema Kawemba.
 Wakati Azam wakiendelea kujivuta kukaa mezani na Wawa, Yanga imekuwa ikifuatilia mchakato mzima na kuna uwezekano beki huyo akatua Jangwani kiulaini tofauti na matarajio ya wengi.

Post a Comment

 
Top