MVUVUMWA FC ya Kigoma inayonolewa na aliyekuwa kocha wa
Geita Gold, Suleiman Matola imeanza vibaya Ligi Daraja la Kwanza baada ya
kufungwa bao 1-0 na Rhino Rangers ya Tabora kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika
mkoani Kigoma.
Matola alisema timu yake ilicheza vizuri katika mchezo huo
lakini bahati haikuwa upande wao na sasa wanajipanga kwa mchezo ujao.
“Sisi tumecheza vizuri lakini wapinzani wetu ndiyo
wameshinda, kulikuwa na makosa kwenye safu yetu ya ushambuliaji tutalifanyia
kazi tatizo hilo kabla ya mchezo ujao,” alisema Matola.
Matola aliongeza kuwa, Mvuvumwa haina uzoefu katika ligi
hiyo ndiyo maana hawakufanya vizuri. “Rhino Rangers wamebebwa na uzoefu wao
katika ligi hii lakini nina imani kuwa timu yangu iko vizuri na tutafanya vema
na hatukati tamaa bali tutapambana mpaka mwisho,” alisema.
Katika matokeo mengine ya ligi hiyo, KMC imeichapa Kurugenzi
FC mabao 3-1, Lipuli imetoka sare ya bao 1-1 na African Sport, Singida United
iliifunga Mgambo JKT bao 1-0 na Polisi Dodoma imeifunga Panone bao 1-0.
Post a Comment