KOCHA wa Yanga, Hans Pluijm amefunguka
kuwa hafurahishwi na kikosi chake kupiga pasi nyingi uwanjani na kutoka bila
pointi.
Yanga ambayo mpaka sasa imecheza mechi
tatu na kati ya hizo imeshinda mbili na sare moja, imekuwa ikisifika kwa kupiga
pasi nyingi huku wanaoongoza kwa kufanya hivyo wakiwa ni Deus Kaseka na Thaban
Kamusoko.
Pluijma amesema anachukizwa na kitendo
cha wachezaji wake kupiga pasi nyingi za nyuma huku pia zikichelewesha wao
kupata ushindi kwani mpira umekuwa ukichelewa kutokana na wao kumiliki mpira
hasa kwenye eneo lao na sio kwenye lango la adui.
“Sikatai kuwa tunatakiwa kucheza soka
la kuvutia lakini muda mwingine soka halina maana sana unaposaka matokeo kwani
kumiliki mpira hakukupi pointi tatu badala yake mabao utakayofunga ndiyo kila
kitu.
‘Tatizo tunapiga pasi nyingi lakini
asilimia kubwa zinakuwa kwenye eneo letu nyingi zikiwa kwa viungo na mabeki
wetu jambo ambalo kwangu naona halina maana kabisa kwani hatufaidiki na uwingi
wa pasi hizo,” alisema
Post a Comment