LEO Jumamosi Azam
FC inacheza ugenini na Mbeya City katika Ligi Kuu Bara, kocha wa timu hiyo Zeben
Hernandez amesema ni lazima washinde leo halafu wajiandae kupata pointi tatu
kwa Simba.
Baada ya mchezo
wa leo na Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya, Azam itarejea jijini Dar
es Salaam kujiandaa na mechi yake dhidi ya Simba itakayochezwa Septemba 17,
mwaka huu.
Azam ina pointi
saba sawa na Mbeya City na timu hizo zimelingana mabao ya kufunga na kufungwa,
hivyo kuleta ushindani wa aina yake katika mchezo wa leo.
Zeben raia wa
Hispania alisema kuwa, anajua mechi ya leo ina presha kubwa kwa timu zote
lakini atahakikisha wanashinda ili kujihimarisha kileleni.
“Tunajua
wapinzani wetu wana kikosi kizuri ambacho kitacheza nyumbani kwa lengo la
kushinda, hili kushusha presha ni lazima tupate matokeo bora tukiwa huku Mbeya.
“Nitahakikisha
tunashinda mechi yetu hii halafu tushinde mechi inayofuata (na Simba) ili tuwe
katika nafasi nzuri zaidi kwenye ligi,” alisema Zeben.
Kwa upande wa
Kocha wa Mbeya City, Kinnah Phiri raia wa Malawi, akizungumzia mchezo huo
alisema: “Tumejiandaa vizuri kwa mechi yetu na Azam na tumejipanga vilivyo
kuhakikisha tunaibuka na ushindi kwani tuna faida ya kucheza nyumbani.
KIKOSI CHA MBEYA CITY |
“Nimewaona Azam
katika mechi dhidi ya Prisons, ni timu nzuri lakini nimeshajua jinsi gani ya
kukabiliana nao na kuwafunga ili tuweze kukaa vizuri kileleni.”
Post a Comment