KOCHA Mkuu wa Yanga,
Hans van Der Pluijm, ametamka kwamba ni lazima wazitumie vizuri nafasi
watakazopata katika dakika 45 za kipindi cha kwanza katika mchezo wao dhidi ya
Mwadui kesho Jumamosi kwa kuwa wamebaini wapinzani wao wengi ni wagumu
kufungika kwenye kipindi cha pili.
Yanga itakuwa kwenye
Uwanja wa Kambarage kukipiga na Mwadui inayonolewa na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’
katika Ligi Kuu Bara ambapo mchezo huo unatajwa kuwa unaweza kuwa mgumu kutokana
na rekodi zao za hivi karibuni.
Mara ya mwisho
zilipokutana kwenye uwanja huo zilitoka sare ya mabao 2-2, safari hii
zinakutana kukiwa na tambo nyingi kutoka kila upande.
Pluijm, kipa wa zamani
wa timu ya taifa ya Uholanzi, amesema kipindi cha pili katika mechi kadhaa kimekuwa
kigumu kwao na wapinzani wengi wamekuwa wakipoteza muda kutafuta sare.
“Hiyo ndiyo mipango yetu, wapinzani wetu wengi kikifika kipindi cha pili wanakuwa hawafungiki kirahisi na wanakaba sana, jambo ambalo linatupa ugumu, pia wanacheza soka la kupoteza muda kwa ajili tu ya kutopata pointi moja,” alisema Pluijm.
Post a Comment