KIKOSI CHA MTIBWA SUGAR
 BAADA ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kutoka kwa Mtibwa Sugar, Kocha Msaidizi wa Kagera, Ally Jangalu, amesema wanahitaji kujitathmini upya.
Matokeo hayo ni kama yameizibua masikio Kagera Sugar,  waliopoteza  mchezo huo juzi kwenye Uwanja wa Manungu, mkoani Morogoro.
Jangalu alisema baada ya kipigo hicho, wanakwenda kujitathimini ili kujua upungufu wa kikosi chao kabla ya kukutana na African Lyon Septemba 25, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Uhuru jijini, Dar es Salaam.
Jangalu alisema walishindwa kuibuka na ushindi kutokana na wachezaji wao kushindwa kutumia nafasi walizozipata katika kufunga mabao.
KIKOSI CHA MTIBWA SUGAR
 “Soka ni mchezo wa makosa, ukishindwa kutumia nafasi, basi mpinzani wako atakuzidi na kuitumia ili kupata matokeo mazuri.
“Tumepoteza mchezo, lakini wachezaji wetu kushindwa kutumia nafasi walizopata kumesababisha wapinzani wetu kuibuka na ushindi, kubwa tunakwenda kujipanga kwa mchezo unaofuata,” alisema Jangalu.
Kagera  wanashika nafasi ya tisa kutokana na  pointi sita, baada ya kucheza michezo mitano, huku Simba wakiongoza kwa pointi 13.

Post a Comment

 
Top