KOCHA
Mkuu wa Simba, Joseph Omog anauchukulia mchezo wao dhidi ya Yanga kama timu
yake inacheza dhidi ya Majimaji tu.
Kauli
hiyo ameitoa ikiwa siku moja kabla ya mchezo wa watani wa jadi wa Simba na
Yanga utakaopigwa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mcameroon
huyo, atakaa benchi kwa mara kwanza katika 'derby' ya Simba na Yanga mechi
inayotarajiwa kujaa upinzani mkubwa kutokana na maandalizi ya kila timu
kuhakikisha wanavuna pointi tatu.
Oog
alisema mechi hiyo anaichukulia ya kawaida kama ilivyokuwa michezo mingine ikiwemo
na Majimaji aliyocheza nayo na kufanikiwa kuifunga mabao 4-0 wikiendi iliyopita.
Aliongeza
kuwa, kwa maandalizi ya timu yake aliyoyafanya yanatosha kabisa kupata ushindi
kwenye mechi hiyo, licha ya wapinzani wao nao kujiandaa.
"Maandalizi
ya timu yapo vizuri kabisa kwa maana ya wachezaji wote wapo kwa ajili ya mchezo
wetu wa Jumamosi, tayari nimemaliza majukumu yangu ya ndani ya uwanja ambayo ni
kuwapa mbinu za ushindi wachezaji wangu.
"Hivyo,
kilichobakia ni kuisubiria mechi yenyewe ambayo presha kubwa ipo kwa mashabiki
lakini siyo kwa wachezaji na benchi la ufundi.
"Nikiwa
kama kocha na wachezaji wangu, tunauchukulia mchezo huo kama michezo mingine
vile ya ligi kuu tunayoicheza ukiwemo na Majimaji tuliyocheza nayo hivi
karibuni," alisema Omog.
Post a Comment