WAKATI Simba na Yanga zikitarajiwa kukutana Oktoba mosi mwaka huu Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, takwimu zinaonyesha kuwa mwezi huo una matokeo mazuri kwa Wanajangwani timu hizo zinapokutana.
Takwimu za miaka ya hivi karibuni zinaonyesha kuwa tangu mwaka 2010 timu hizo zilipokutana, Simba wamekuwa wakipata wakati mgumu kupata matokeo mazuri ambapo ushindi wao umekuwa ni sare.
Msimu huo wa mwaka 2010/11 timu hizo zilipokutana Oktoba 16, Yanga walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0, likifungwa na Jerryson Tegete Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.
 Msimu wa 2011/12 timu hizo zilipokutana jijini Dar es Salaam, Yanga walifanikiwa tena kuibuka na ushindi wa bao 1-0, lililofungwa na Mzambia Davis Mwape katika dakika ya 75, ndipo Simba walipomalizia hasira mzunguko wa pili wakishinda mabao 5-0.
 Msimu wa 2012/13 timu hizo zilipokutana Oktoba 3 zilitoka sare ya kufungana bao 1-1, bao la Simba likifungwa na Amri Kiemba na lile la Yanga likikwamishwa wavuni na Said Bahanuzi.
 Oktoba 20, 2013, timu hizo zilitoka sare ya kufungana mabao 3-3, Yanga wakitangulia kufunga mabao yao kipindi cha kwanza na Simba kusawazisha yote kipindi cha pili, mabao ya Yanga yakifungwa na Mrisho Ngasa na Hamis Kiiza aliyefunga mawili, huku ya Simba yakifungwa na Betram Mwombeki, Joseph Owino na Gilbert Kaze.
Msimu wa mwaka 2014/15 timu hizo zilipokutana Oktoba 18 zilitoka suluhu ya 0-0, ambapo msimu uliopita hazijakutana Oktoba na badala yake zilikutana Septemba na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Post a Comment

 
Top