JUMAMOSI hofu kubwa ilitawala kwa mashabiki wa
Simba baada ya kushuhudia fowadi matata, Ibrahim Ajib akilazimika kupumzishwa mapema
kunako dakika ya 28, kwa ushauri wa idara ya matibabu, chini ya daktari, Yassin
Gembe baada ya kuumia wakati wa mchezo dhidi ya Majimaji.
Ajibu alilazimika kumpisha Said Ndemla muda huo
baada ya kuumia mguu lakini mara baada ya mchezo, nyota huyo maarufu kama
Cadabra, aliliambia Championi Jumatatu kuwa, yupo fiti na wala mashabiki wasiwe
na hofu yoyote ya kukosekana kwenye mchezo ujao dhidi ya watani, Yanga.
Cadabra ambaye amekuwa tegemeo la mabao ya Simba
kwa kiasi kikubwa, yeye na Shiza Kichuya, wakati anatoka uwanjani, mashabiki wa
Simba walionekana kuwa na hofu kubwa ya kukosekana kwenye mchezo wa wikiendi
hii lakini mwenyewe alipoulizwa alisema:
“Nipo fiti, sijaumia kihivyo, kidogo tu na nitacheza kama nikipangwa siku
hiyo.”
Post a Comment