NAHODHA wa Azam, John Bocco na yule wa Simba, Jonas Mkude, wametambiana huku kila mmoja akidai kuwa timu yake ndiyo itaibuka na ushindi wakati klabu hizo zitakapokutana kesho kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Wakizungumza na spotiripota kwa nyakati tofauti wachezaji hao kila mmoja alikiri kuwa mchezo huo utakuwa mgumu, lakini pia walitamba kuwa wataibuka na ushindi.


Kwa upande wake Mkude alisema mechi itakuwa ngumu kwani kila timu inahitaji pointi tatu lakini wanaendelea kujifua na matumaini yao ni kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo.
“Tumejiandaa vizuri na mchezo huo na tunaendelea kujiandaa kwa ajili ya kuibuka na ushindi kwenye mechi hiyo licha ya kutambua ugumu uliopo kwani Azam ni timu nzuri na ipo kwenye nafasi ya juu katika msimamo wa ligi.” alisema.

Naye nahodha wa Azam, John Bocco, alisema timu yao ina morali kubwa ya kuibuka na ushindi katika mechi hiyo na wanaendelea na maandalizi kutoka kwa makocha wao.
“Tumejiandaa vizuri na tunajipanga kwenda kuchukua pointi tatu dhidi ya Simba, wachezaji wana ari ya mchezo na tutakwenda kupambana,” alisema

Post a Comment

 
Top