NAHODHA wa Simba, Jonas Mkude,
amesema hawezi kuizungumzia sana mechi yao dhidi ya Yanga, kwani
anaamini dakika 90 za mchezo huo ndizo zitakazoamua nani mshindi kwenye
pambano hilo.
Yanga na Simba zitashuka dimbani
Oktoba mosi mwaka huu kuumana katika pambano litakalopigwa kwenye Uwanja wa
Taifa.
Mkude alisema anaamini Yanga
wanafanya maandalizi ya nguvu kwa ajili ya mchezo huo kama ilivyo wao, hivyo
hawezi kuuzungumzia sana zaidi ya kusubiri muda ufike.
“Yanga wanajiandaa na sisi
tunajiandaa pia, mechi itakuwa ngumu kutokana na kila mmoja kuhitaji ushindi
ili kujiongezea pointi na kulinda heshima, lakini naamini dakika za mchezo huo
ndizo zitaamua nani ataibuka kidedea dhidi na mpinzani wake,” alisema.
Simba kwa sasa wameshikilia usukani
wa ligi hiyo wakiwa na pointi 16, baada ya kucheza mechi sita, huku wakiibuka
na ushindi kwenye michezo mitano na sare moja.
Yanga wapo katika nafasi ya tatu
wakiwa na pointi 10 baada ya kucheza mechi tano, wakishinda mechi tatu,
sare moja na kupoteza mchezo mmoja.
Post a Comment