KIUNGO na nahodha wa Simba, Jonas
Mkude amesema huu si wakati wa kutamani mafanikio ya wapinzani wao, Yanga ya
kushiriki michuano ya kimataifa, bali ni kuhakikisha wanapambana na kupata
nafasi hiyo msimu ujao.
Kauli hiyo ya Mkude imekuja siku
chache baada ya Simba kuifunga Ruvu Shooting mabao 2-1 katika mechi ya Ligi Kuu
Bara iliyochezwa Jumatano wiki hii kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mkude alisema Simba inapambana ili iweze
kufanya vizuri katika michezo yake na kutimiza malengo waliyojiwekea na siyo
kuanza kusikilizia matokeo ya Yanga.
“Kiukweli ligi imeanza kuonekana kuwa
ngumu mapema kabisa kwa sababu kila timu inahitaji ushindi na sisi tunachokifanya
kwa sasa ni kuhakikisha tunapata ushindi katika kila mchezo ili tuweze kufikia
malengo tuliojiwekea ikiwemo kushiriki michuano ya kimataifa.
“Huu siyo wakati wa kuangalia kila
kitu ambacho kinafanywa na wapinzani wetu zaidi ya sisi kuanza kutengeneza ya
kwetu ili tuweze kufika walipofika wao,” alisema Mkude.
Post a Comment