KIUNGO wa zamani wa Yanga, Andrey Coutinho amerejea Dar na kusema anatamani kurejea kikosini humo kwani anaipenda.
Coutinho raia wa Brazil amesema: “Nimemaliza mkataba wangu na klabu ya Rakhine United ya Myanmar  ambayo ilikuwa inashiriki ligi kuu. Huko nilifunga mabao 10 na sasa nipo hapa Tanzania nimeletwa na kiongozi wa Yanga.
 “Nitakuwa hapa nchini kwa siku tano pekee nitakuwa namazungumzo na bosi wa Yanga. Ninavutiwa na wachezaji waliopo kama Kamusoko, na Niyonzima, hao ndiyo wananivutia zaidi uchezaji wao na wananifanya nipende kurehea Yanga. Ukisikia ninarejea kucheza soka Bongo basi tambua ni Yanga na sio timu nyingine.
 “ Nimesikia Yanga wanacheza Jumamosi hivyo nitaenda uwanjani kuwaangalia,” alisema Coutinho ambaye pia amepanga kwenda kuwasalimia wachezaji wenzake kwenye mazoezi ya timu hiyo.  

Post a Comment

 
Top