WAKATI homa ya
pambano kati ya Azam FC dhidi ya Simba litakalopigwa kesho Jumamosi kwenye
Uwanja wa Uhuru, badala ya Uwanja wa Taifa ikizidi kupanda, Simba
haijafurahishwa na maamuzi hayo, imeripotiwa kuwa wamekuwa wakifanya bidii
kushawishi mabadiliko ya uwanja.
Mchezo huo ambao Azam
FC ndiyo wenyeji, ulipangwa kufanyika Taifa lakini kutokana na uwanja huo
kutumiwa na timu ya taifa ya vijana ya Congo Brazzaville (U-17) kesho Jumamosi
kufanya mazoezi ya mwisho kujiandaa na mchezo dhidi ya Serengeti Boys, Jumapili
kama sheria ya Fifa inavyosema, ikalazimu kufanyika kwa mabadiliko hayo.
Inadaiwa kuwa Simba inahofi
a kupoteza mchezo huo kwa kuwa wachezaji wao bado hawajazoea nyasi za Uwanja wa
Uhuru ambazo ni za bandia wakati Azam wao wanao uwanja wa nyasi bandia.
Hadi jana Alhamisi jioni
viongozi kadhaa wa Simba walikuwa wanafanya kila liwezekanalo kuishawishi Congo
kuutumia Uwanja wa Taifa, leo Ijumaa kwa mazoezi ya mwisho badala ya kesho ili waweze
kuutumia.
Aidha, mtu wa ndani
wa TFF amethibitishia kuwepo kwa kampeni hiyo ya Simba kwani wanajua nyasi bandia
ni faida kwa Azam ambao wamezoea nyasi hizo kuanzia mazoezini mpaka kwenye
mechi nyingi.
“Lakini sidhani kama
mpango wao unaweza kukubalika kwa muda uliobaki na sidhani kama Congo wenyewe
wanaweza kuwakubalia.
“Kumbuka wamekuja kucheza mechi ya
mwisho kufuzu Fainali ya Mataifa Afrika, siamini kabisa,” alisema kigogo mwenye
hadhi kubwa ndani ya TFF.
Alipotafutwa Mratibu
wa Simba, Abbas Ally ‘Gazza’ alisema: “Sina hizo taarifa na kazi yangu ni
kuiandaa timu kuona inafanya vizuri. Kama ni maamuzi ya kutupeleka Uwanja wa
Uhuru sisi tumeridhika.”
Post a Comment